Kuhusu BUM

Bodi ya Utangazaji ya Magavana (BUM) ni jina la shirika huru la shirikisho ambayo inasimamia vyombo vya habari vya kimataifa vya raia wote wa Marekani na jina la bodi ambayo inaongoza matangazo hayo.

Ujumbe wa BUM ni kuwajulisha, kujihusisha na kuunganisha watu duniani kote kuunga mkono uhuru na demokrasia. Kila wiki, Zaidi ya milioni 226 ya wasikilizaji, watazamaji, na watumiaji wa intaneti duniani hufungua, kusikiliza, na kuingia programu za matangazo ya kimataifa ya Marekani.

Wakati Bodi ya Utangazaji wa Magavana nijina la kisheria kwa chombo cha shirikisho linalozunguka huduma zote za matangazo ya kimataifa ya Marekani, shughuli za kila siku za utangazaji zinafanywa na watangazaji wa kimataifa wa kibinafsi wa BUM: Sauti ya Marekani (SYM), Redio Huru ya Ulaya/ Redio Huru (RHU/RH), Redio Huru ya Asia (RHA), Redio na Televisheni Martí na Alhurra, Redio Sawa, kwa msaada wa Shirika la Kimataifa la Utangazaji (SKU).